Msimamao wa Cord: Serikali ya Jubilee imefeli kwa mambo mengi
9th April, 2016
Muungano wa upinzani nchini cord umekosoa hotuba ya Rais Kenyatta kwa taifa ukisema kuwa aliwapotosha wakenya. Wakiongozwa na Raila Odinga, Kalonzo Musyoka na Moses Wetangula cord imesema kuwa serikali ya jubilee imefeli kwa sekta nyingi kama vile usalama na utalii. Kalonzo musyoka amesema kuwa tume huru ya uchaguzi na mipaka haitakiwi kusimamia uchaguzi mkuu ujao.