Kilio cha mwathiriwa wa ghasia za baada ya uchaguzi.
7th April, 2016
Walter Barasa mmoja wa watu wanaotafutwa na mahakama ya ICC kwa madai ya kuvuruga ushahidi dhidi ya waliokuwa washukiwa wakuu wa ghasia za baada ya uchaguzi, amejitokeza mapema leo na kudai kwamba haogopi kukamatwa na maafisa wa icc. Vile vile Barasa amemshtumu mwendeshaji mashataka Fatou Bensouda kwamba alishindwa kupata ushahidi dhidi ya naibu wa rais William Ruto na mwanahabari Joshua Sang na badala yake ameelekeza hasira yake kwa samaki wadogo wasiokuwa na hatia.