Madai ya polisi kuwapija mijeledi wanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi yaibua hisia kali
5th April, 2016
Madai ya polisi kuwapija mijeledi wanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi wakati wa ghasia za chuoni humo yanazidi kuibua hisia mbalimbali huku tume ya kutetea haki za binadamu ikitoa msimamo wake kuhusu suala hilo. Mapema hivi leo, msemaji wa polisi alipuuza video iliyoashiria polisi wakiwapa wanafunzi funzo la viboko barabarani lakini baadaye, tume ya haki za binadamu ikasema imearifiwa kuhusu sio viboko tu mbali pia tuhuma za ubakaji na ipo kwenye uchunguzi wa madai hayo. Chuo kikuu cha nairobi nacho kimefungwa kwa muda usiojulikana kufuatia ghasia hizo.