Ghasia zazuka katika mkutano wa Wetangula
2nd April, 2016
Ghasia zilizuka katika mkutano wa kisiasa huko kakamega ambapo kiongozi wa ford kenya Moses Wetangula alitangaza kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao. Mtu mmoja alijeruhiwa katika vurugu hizo na kusababisha wasiwasi mkubwa.polisi walilazimika kuwatawanya wafuasi kabla ya kurejesha hali. Mkutano huo ulihudhuriwa na mmoja wa vinara wa cord Kalonzo Musyoka.