Kimani Ngunjiri: wabunge wa upinzani walikosea kumzomea rais Kenyatta
1st April, 2016
Mbunge Wa Bahati Kimani Ngunjiri amewashutumu wabunge wa upinzani waliojaribu kuvuruga hotuba ya Rais Uhuru Kenyatta bungeni hapo jana. Akizungumza huko Nakuru Ngunjiri alisema kuwa wabunge hao walitoa mfano mbaya mno kwa taifa. Baadhi ya wabunge wa mrengo wa cord walimtatiza Rais Kenyatta hapo jana na kumlazimu spika wa bunge kuwaondoa baadhi yao nje ya bunge