Nkaissery aangazia swala la Joho
12th March, 2016
Waziri wa usalama wa ndani Joseph Nkaissery amekariri kuwa walinda usalama wa gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho walipunguzwa akitaja alikuwa na wengi kupita kiasi. Haya yanajiri huku viongozi tofauti wakiendelea kutoa hisia tele kuhusu kupunguzwa kwa maafisa wa usalama kwa gavana wa Kilifi Amason Kingi na gavana wa mombasa ali hassan joho.