Wario alaumiwa kwa kupuuza vipenge muhimu vya kisheria
10th March, 2016
Kamati ya bunge inayohusika na masuala ya jamii na ajira amemnyoshea kidole cha lawama waziri wa michezo Dkt Hassan Wario kwa kupuuza vipengee muhimu vya kisheria alipounda jopo la kushughulikia janga la utumizi wa dawa zilopigwa marufuku kwa wanariadha kufuatia amri ya Rais Uhuru Kenyata. Kamati hiyo ilikuwa ikijadili ombi lilotolewa na mbunge wa cherangany ambaye pia ni mshindi wa mbio za Boston mwaka 2012 Wesley Korir ili kuafikia makataa ya tarehe tano mwezi aprili.