Wakulima eneo la kaskazini mwa bonde la ufa waingiwa na hofu kufuatia upungufu wa mbolea
9th March, 2016
Wakulima katika eneo la kaskazini mwa bonde la ufa wameingiwa na hofu kufuatia upungufu wa mbolea. Wakulima hao wanadai ingawa mvua imeanza kunyesha wakiwa wametayarisha mashamba yao kwa ajili ya msimu wa upanzi, upungufu wa mbolea unatishia kuathiri mazao yao baadaye.