Jumba lenye orofa 4 laporomoka mtaani Zimmerman, jijini Nairobi
9th March, 2016
Jumba lenye orofa 4 mtaani Zimmerman limeporomoka usiku wa kuamkia leo. Kulingana na wakaazi jumba hilo liliporomoka mwendo wa saa nane usiku wa kuamkia leo huku maafisa wa usalama na wale wa msalaba mwekundu wakiwa bado wanaendeleza shughuli za uokozi.