Mkuu wa COTU Francis Atwoli atoa wito kwa Waluhya kuwajibika
5th March, 2016
Katibu mkuu wa muungano wa wafanyikazi nchini Francis Atwoli ameitaka jamii ya waluhya kujisajili kama wapiga kura na kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu ujao. Atwoli amesema kuwa waluhya ni wengi lakini ukosefu wa umoja umewanyima nafasi ya kuongoza. Alisema hayo huko kwisero.