Vuguvugu la MRC lawahimiza wanachama kujiandikisha kuwa wapiga kura uchaguzi mkuu unapokaribia
1st March, 2016
Vigogo wa vuguvugu la MRC sasa wanawataka wanachama wao kujitokeza na kujiandikisha kuwa wapiga kura uchaguzi mkuu unapokaribia…..haya yanajiri baada ya viongozi wa kundi hilo kukubali kukutana na wasimamizi wa tume ya uchaguzi nchini IEBC kuendesha uhamasisho wa usajili.