Vurugu yazuka katika shughuli ya kuandikisha wapiga kura mtaani Kariobangi
1st March, 2016
Kulizuka vuruga mtaani Kariobangi jijini Nairobi huku wakazi wakilalamikia kile walichotaja kama uhamisho wapiga kura kutoka maeneo mengine kuja kujisajili huko. Fujo hizi zinajiri siku tatu tu baada ya ya usajili wa wapiga kura wapya kuanza katika shule ya maruru mtaani humo. Shughuli hiyo ilisitishwa na ilibidi polisi waingilie kati kukomesha makabiliano.