Katibu wa COTU Francis Atwoli akashifu wanaojihusisha na ufisadi nchini
29th February, 2016
Katibu mkuu wa muungano wa vyama vya wafanyikazi nchini COTU, Francis Atwoli amekashifu wale wanaojihusisha na ufisadi nchini akisema ongezeko la ufisadi limewakosesha vijana wengi kazi.. Atwoli alisema haya baada ya kurejea kutoka Algeria ambapo juhudi zake za kupigania haki za wafanyikazi barani Afrika zilimwezesha kutunikiwa heshima ya kipekee na rais wa Algeria Abdelaziz Boute-Flika inayofahamika kama highest distinction.