Wakaazi wa kijiji cha Waon, Elgeyo Marakwet wahofia maisha yao kufuatia visa vya kuumwa na majoka
28th February, 2016
Wakazi wa kijiji cha Waon katika kaunti ya Elgeyo Marakwet wanaishi na roho mikononi kufuatia visa vya kuumwa na majoka hatari. Maafisa wa afya katika kaunti hiyo wamedai kuwa zaidi ya wakazi wawili huumwa na nyoka kila wiki katika msimu huu wa kiangazi.