Kampeni za Useneta zapamba moto katika Kaunti ya Kericho
26th February, 2016
Naibu rais William Ruto amezuru eneo la Kericho kumpigia debe mgombezi wa chama cha JAP Aaron Cheruiyot huku siasa za uchaguzi mdogo wa useneta wa Kericho zikizidi kushika kasi. Ruto alijumuika na wanasiasa kama Magerer Langat, waziri Charles Keter, seneta Kipchumba Murkomen na waziri wa zamani Franklin Bett. Wote walielezea uhakika wa mgombezi wao kuibuka mshindi huku mirengo tofauti ya kisiasa eneo la Rift Valley ikipigia debe mgombezi wao.