Mbio za First Lady Marathon kuandaliwa Machi 6
25th February, 2016
Mkewe wa rais Bi Margaret Kenyatta huenda akashiriki mbio za kilomita kumi wala sio za kilomita 21 kama ilivyo desturi yake katika makala ya tatu ya mbio za mashindano ya first lady half marathon yatakayofanyika tarehe 6 mwezi ujao. Ikiwa imesalia takriban juma moja tu kabla ya mashindano hayo kufanyika, Bi Margaret Kenyatta alifanya mazoezi leo asubuhi katika uwanja wa kasarani.