Rais Kenyatta asalimu amri na kuteua jopo la kuchunguza jaji Philip Tunoi kwa tuhuma za ufisadi
23rd February, 2016
Rais Uhuru Kenyatta hatimaye amemsimamisha kazi kwa muda jaji wa mahakama ya juu anayetuhumiwa ulaji mlungula na kuteuwa jopo la kuchunguza tuhuma zinazomkabili. Hatua ya rais imechukuliwa siku moja tu baada ya msimamizi wa shughuli za rais Joseph Kinyua kutuma waraka akisema rais hatateuwa jopo kwa sasa.