Rais Uhuru Kenyatta adinda kuteua jopo maalum la kuchunguza Jaji Philip Tunoi kwa madai ya ufisadi
22nd February, 2016
Rais Uhuru Kenyatta hatoteuwa jopo maalum la kuchunguza madai yanayomkumba jaji wa mahakama ya juu Philip Tunoi. Kwenye waraka rasmi kwa vyombo vya habari na tume ya huduma kwa mahakama JSC ikulu ya Nairobi imesema kwamba jaji Tunoi tayari ana kesi mbele ya mahakama ya rufaa kuhusu muhula wake wa kudumu.