Riadha ya chipukizi kufanyika Kasarani
18th February, 2016
Mashindano ya dunia ya riadha ya chipukizi yataandaliwa katika uwanja wa Kasarani wala si nyayo kama ilivyokuwa ikifahamika hapo awali. Hii ni kutokana na ukarabati ambao utahitajika endapo mashindano hayo yataandaliwa Nyayo. Japo muda unayoyoma, kamati unayohusika na maandalizi ina imani kuwa kila kitu kitakuwa shwari.