Vyama vya siasa visiwani Zanzibar vyatishia kususia uchaguzi wa marudio
14th February, 2016
Vyama vya siasa visiwani Zanzibar vimesema kuwa vitasusia uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika tarehe 20 mwezi machi mwaka huu. Vyama hivyo vilishiriki uchaguzi wa octoba 25 mwaka jana uliofutiliwa mbali na tume ya uchaguzi nchini humo. Wawakilishi wa vyama hivyo wanadai kuwa uchaguzi huo hautakuwa huru.