x News The Standard Digital KTN Prime KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS Tutorsoma Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
x
x

Watu saba wafariki kwenye ajali huko Mairiakani kaunti ya Mombasa

13, Feb 2016

Watu saba wamepoteza maisha yao hii leo baada ya matatu waliyokuwa wakisafiria kuhusika katika ajali eneo la bonje mariakani kwenye barabara kuu ya Mombasa kuelekea nairobi.matatu hiyo iliyokuwa ikitoka Mombasa kuelekea Voi, iligongana ana kwa ana na lori. Watu watano walifariki papo hapo huku wengine wawili wakifariki pindi tu walipofikishwa katika hospitali ya mariakani. Wanne kati ya waliofariki ni wanawake na watatu ni wanaume. Inaaminika kuwa lori husika lilipoteza mwelekeo wakati ambapo magari hayo yaligongana. Kaimu OCPD wa eneo la kaloleni Patrick Ngeiywa amesema kuwa uchunguzi umeanzishwa kubaini chanzo kamili cha ajali hiyo. Eneo hilo la bonje limetajwa na maafisa wa usalama kama hatari zaidi na waendeshaji magari wametakiwa kuwa waangalifu wanapotumia sehemu hiyo ya barabara. Watu watatu waliojeruhiwa wanaendelea kupata matibabu katika hospitali ya mariakani.

Feedback