Wabunge Alfred Keter na Olago Aluoch waikosoa EACC kwa kumwondolea lawama Ann Waiguru
8th February, 2016
Baadhi ya wanasiasa wameukosoa uamuzi wa tume ya kupambana na ufisadi nchini kwa kumwondolea lawama aliyekuwa waziri wa ugatuzi Anne Waiguru ambaye alikuwa anakabiliwa na tuhuma za ufisadi. Wabunge Alfred Keter na Olago Aluoch wanasema tume hiyo imezima azma ya kupambana na ufisadi nchini.