NYEMBE ZA UKEKETAJI: Juhudi za kupambana na ukeketaji
6th February, 2016
Visa vya ukeketaji miongoni mwa jamii nchini kenya,vimetajwa kushuka kwa kiasi hasa baada ya serikali kubuni tume maalum ya kupiga vita dhulama hizo kwa ushirikiano na mashirika ya kijamii. Kulingana na ripoti ya afya mwaka 2015, matokeo yameashiria upungufu ingawa kuna ongezeka kwa baadhi ya kaunti nchini Kenya. Ali manzu alizuru sehemu ya kaskazini mashariki ya kenya,ambako kuna ongezeko la asilimia 94 ya ukeketaji na kupata na muathiriwa mmoja ambaye sasa anaitaka jamii ya wasomali kuachana na tabia hio iliopitwa na wakati.