Bodi yakamata wahudumu wafamasi bandia Kayole
6th February, 2016
Bodi kuhusu dawa na sumu nchini imewakamata wahudumu bandia 26 katika mtaa wa Kayole hapa jijini Nairobi. Baadhi ya waliokamatwa hawakuwa na leseni za kumiliki maduka ya kuuza dawa. Kadhalika wengine walikuwa wanauza dawa ambazo zinatakiwa kutolewa bila malipo.