Viongozi kutoka jamii ya Maasai wahimiza vijana wa kimorani kujisajili kupata vitambulisho
3rd February, 2016
Viongozi kutoka jamii ya Maasai katika kaunti ya Kajiado,wamewataka vijana wa kimorani kujisajili kupata vitambulisho na kadi za kura na kushiriki katika uendelezaji wa shughuli za taifa. Wakizungumza katika eneo la Kajiado kusini,mbunge wa Kajiado kusini Katoo ole Metito na aliyekuwa waziri Joseph ole Lenku wameungana na viongozi wengine wa jamii kuwashikiza vijana na hata wazee kujisajili.