Wafanyakazi mradi wa reli wa Standard Gauge wagoma Syokimau kulalamikia malipo duni
2nd February, 2016
Wafanyakazi kwenye mradi wa reli wa Standard Gauge eneo la Syokimau wamegoma leo ikiwa ni mara ya tatu katika kipindi cha chini ya wiki moja wakilalamikia malipo duni na hali mbaya ya kazi. Wafanyakazi hao waliandamana kwenye barabara kuu ya Mombasa kabla ya kutawanywa na polisi mapema hivi leo.