Dhuluma shuleni: Mwanafunzi mmoja auawa baada ya kupigwa na mwalimu
22nd January, 2016
Polisi katika eneo la Kieni kaunti ya Nyeri wanasubiri matokeo ya upasuaji wa mwili wa mwanafunzi mmoja wa darasa la sita ili kubaini iwapo ni kweli mtoto huyo alipigwa na mwalimu wake hadi akafariki. Kevin Kagurua aliadhibiwa na mwalimu mmoja siku ya jumatano adhuhuri, na kuzirai kabla ya kuripotiwa amefariki.