Washukiwa wanne wa ugaidi wauawa mjini Malindi
20th January, 2016
Huku Kenya ikiendelea kuomboleza vifo vya wanajeshi wake walioshambuliwa nchini Somalia, vita dhidi ya ugaidi vimeonekana kupamba moto humu nchini. Hii ni baada ya polisi mjini Malindi kuwapiga risasi na kuwaua washukiwa wanne wa ugaidi asubuhi ya leo kwenye kijiji cha kwa chocha eneo hilo. Silaha kama magurunedi, ramani zinazoonyesha vituo vya ulinzi sehemu za lamu,malindi na garissa na vifaa vya mawasiliano vilipatikana kwao.