Gavana wa Machakos Alfred Mutua awakashifu wanaopinga vuguvugu la Maendeleo Chap Chap
6th January, 2016
Gavana wa Machakos Alfred Mutua amewakashifu wapinzani wake wanaopinga vuguvugu la Maendeleo Chap Chap. Mutua anatoa kauli hii siku chache baada ya kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka kumtaka ajiondoe chamani kutoa nafasi kwa uchaguzi mdogo wa kiti cha ugavna katika kaunti ya Machakos. Kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa yeyote anayehama chama afaa kujiuzulu wadhifa wake