Elimu na Taalum: Wataalam wapongeza hatua ya kutoorodhesha wanafunzi, shule kwenye mtihani wa KCPE
4th January, 2016
Kwa mara nyengine tena wizara ya elimu haikuorodhesha wanafunzi wala shule bora kwenye mtihani wa kitaifa wa KCPE. Hatua hiyo yatokana na sera zilizoanzishwa mwaka jana. Wataalam wa elimu wamepongeza hatua hiyo wakisema inapunguza dhana inayoyafanya masomo kuwa ushindani badala ya kuwa njia ya kupata maarifa . Ndilo suala tunaloangazia leo kwenye elimu na taalum.