Hali ya utulimvu yarejea Olposimoru Narok baada ya uhasama baina ya jamii za Wakipsigis na Wamaasai
28th December, 2015
Hali ya utulimvu imerejea katika eneo la Olposimoru kaunti ya Narok baada ya kuwepo kwa uhasama baina ya jamii za Wakipsigis na Wamaasai. Pande hizo mbili hatahivyo zimekubaliana kudumisha amani baada ya mikutano kufanywa na vyombo vya usalama. Kufikia sasa idadi ya wale walioathirika na kufurushwa makwao imeongezeka hadi 700 huku shirika la msalaba mwekundu likiwasaidia na misaada.