Huzuni imewatanda jamaa walioshirikiana na Ahmed Darwesh kwa shughuli zake za kihisani
19th December, 2015
Huzuni ingali imewatanda jamaa waliokua wakishirikiana na mwanahabari Ahmed Darwesh katika shughuli zake za kihisani katika sehemu ya maumba, huko Shimba Hills kaunti ya Kwale. Katika hafla ya kuwazawadi wanafunzi wa madrasa aliokuwa akiisimamia marehemu, Wanafunzi hao walimtaja marehemu kuwa mtu wa watu ambaye alijali jamii kupitia wakfu wa Ahmed Darwesh.