MAANA YA ITIKADI: Mila hupalilia uwajibikaji katika Kaunti ya Nyeri
6th December, 2015
Je yawezekana kwa itikadi ya tohara kurejelea mfumo wake wa awali sawa na ilivyokuwa kabla ujio wa mkoloni ? Majuzi imefanyika sherehe ya tohara katika eneo la kati mwa nchi huku wazee wakisema mojawapo ya mambo yanayochangia katika kizazi cha kisasa cha wanaume kutowajibika ni ukiukaji wa desturi asili.