“Chuo cha Garissa lazima kifunguliwe haraka iwezekanavyo” asema Naibu wa Rais William Ruto
6th December, 2015
“Chuo cha Garissa lazima kifunguliwe haraka iwezekanavyo” ndio kauli ya Naibu wa Rais William Ruto alipozuru chuo hicho. Aidha Ruto amesema kutoendelea masomo katika chuo cha Garissa ni ishara ya kutangaza ushindi kwa kundi la Alshabaab. Wasimamizi wa Chuo Cha Moi na waziri husika wamepewa muda wa wiki mbili zijazo ili kuhakiksha kuwa shughuli za chuo hicho zimeanza kama ilivyokuwa hapo awali.