Wakazi washerehekea minofu ya nyama ya Kiboko aliyeuawa na maafisa wa KWS Nyahururu
4th December, 2015
Wakazi wa kijiji cha Losogwa huko Nyahururu wamesherehekea minofu ya nyama ya Kiboko baada ya maafisa wa KWS kumuua Kiboko huyo anayedaiwa kuharibu mazao ya mashambani mwao. Punde tu baada ya kuuawa kwa kiboko huyo wenyeji waliuchangamkia mzoga wake na kuufanya kuwa kitoweo.