Seneti yaidhinisha ripoti kumfuta kazi afisa mkuu wa KQ Mbuvi Nguze
3rd December, 2015
Seneti imeidhinisha ripoti ya kamati iliyochunguza masaibu ya shirika la ndege la Kenya Airways imependekeza kuwa afisa mkuu wa shirika hilo Mbuvi Nguze afutwe kazi na pia kupendekeza kuchunguzwa upya kwa aliyekuwa afisa mkuu wa KQ Titus Naikuni. Kamati hiyo inayoongozwa na seneta wa Kisumu Anyang Nyongo imependekeza kutimuliwa kwa mameneja wakuu kabla ya serikali kutoa fedha za kulifadhili shirika hilo ambalo limepata hasara ya shilingi bilion 33.9