Je Wakenya wamejiandaa kivipi kumpokea Papa Francis?
25th November, 2015
Baba mtakatifu anatarajiwa nchini. Kwa mujibu wa wapanda ratiba ya Papa Francis ndege yake itatua katika uwanja wa JKIA saa kumi jioni, Idara ya Polisi imetoa orodha maalum ya barabara zitakazofungwa kesho alasiri hadi siku ya mwisho ya ziara ya Papa humu nchini. Miongoni mwa barabara hizo ni Uhuru Highway, Waiyaki Way, Mizunguko ya Bunyala na wa Globe.