Mto Nyando wavunja kingo zake na kuwaacha mamia ya wakaazi bila makao
17th November, 2015
Mamia ya wakaazi wa kijiji cha maembeni eneo la Ahero kaunti ya Kisumu wameachwa bila makao baada ya Mto Nyando kuvunja kingo zake mapema leo nyakati za asubuhi. Mto huo haukosi kuvunja kingo wakati wa mvua na kuathiri makazi na shughuli za wenyeji karibu yake.