Gor Mahia kuzima stima kwa bao 1-0
28th October, 2015
Mabingwa wa ligi kuu ya soka nchini Gor Mahia wameendeleza msururu wa kutoshindwa msimu huu baada ya kuzima stima
Gor Mahia waliotia kibindoni taji hili bado haijapoteza mchuano wowote na huku mchuano huu ukionekana kutamatika ya sare tasa, kiungo wao wa mbele Michael Olunga alipachika bao hilo la pekee dhidi ya Western Stima kunako dakika ya 87.mchuano huo ulichezea ugani Moi Kisumu.