Mwanamke aliyetekwa nyara katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab anusuriwa akiwa hai
16th October, 2015
Mwanamke aliyetekwa nyara siku nne zilizopita katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab amepatikana akiwa hai. Judy Mutua mwenye umri wa miaka 27 alipatikana mjini Dobley nchini Somalia akivushwa kwa lazima hadi Somalia. Vikosi vya usalama vya Kenya vilisaidaina na jeshi la Somalia kumnusuru.