×
× KTN KTN News KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified Jobs Games Crosswords Sudoku The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login
×
Show Swahili

Msemaji wa polisi Masoud Mwinyi,wengine 63 wasimamishwe kazi kwa madai ya ufisadi

15th October, 2015

Msemaji wa polisi wa utawala nchini Kenya Masoud Mwinyi ni miongoni mwa maafisa 63 wa polisi ambao tume ya huduma kwa polisi inapendekeza wasimamishwe kazi kwa muda kwa madai ya kuhusika na ufisadi. Tume hiyo imetoa pendekezo hilo baada ya kuwakagua maafisa 1,300 kwa kipindi cha miezi 14. Baadhi ya maafisa ambao tume hiyo inasema wanastahili kuachishwa kazi ni polisi wa trafiki. Mwenyekiti wa tume hiyo Johnston Kavuludi amesema kuwa wakati wa ukaguzi huo waligundua kwamba maafisa wa vyeo vya chini wanaofanya kazi katika idara hiyo huwagawia fedha za hongo wakubwa wao katika idara ya polisi.
.
RELATED VIDEOS