Serikali yatoa shilingi Bilioni Kumi na Moja kwa mpango wa elimu bila malipo kwa shule za umma
14th October, 2015
Serikali hatimaye imetoa shilingi Bilioni Kumi na Moja kwa mpango wa elimu bila malipo kwa shule za umma. Fedha hizo hata hivyo zimetolewa baada ya wakuu wa shule za Sekondari kulalamikia kuchelewa kwa kifungu hicho, hali ambayo ilitishia kulemaza bajeti ya mitihani ya kidato cha nne inayoendelea kote nchini. Mwenyekiti wa chama cha wakuu wa shule za sekondari John Awitti amesema kwamba kukosekana kwa fedha hizo kuliwapa wasiwasi wakuu wa shule, kutokana na ukosefu wa vifaa vilivyohitajika kununuliwa kwa ajili ya mitihani ya sayansi, inayofanywa katika maabara, yaani practicals