Mahakama ya rufaa yatupilia mbali ombi la kubadilishwa kwa majaji wanaosikiza rufaa ya walimu
29th September, 2015
Na huku watahiniwa wa KCPE na KCSE wakihangaika nchini, hapa jijini Nairobi serikali na walimu wameendeleza zogo lao mahakamani. Mahakama ya rufaa imetupilia mbali ombi la kubadilishwa kwa majaji wanaosikiza rufaa ya tume ya huduma za walimu…. Mawakili wa chama cha KNUT walikuwa wameomba kwamba majaji wapya wateuliwe kusikiliza rufaa hiyo ili kuondoa mwingilio wa serikali.