Mahakama Kuu yasitisha dhamana iliyotolewa kwa mshukiwa wa ulanguzi wa pembe za ndovu
24th August, 2015
Mahakama kuu imesitisha dhamana iliyotolewa kwa mshukiwa wa ulanguzi wa pembe za ndovu Feisal Mohamed hadi pale jaji atakapotoa uamuzi kuhusu iwapo dhamana ya hakimu siku ya Ijumaa ni halali au la . Hii itakuwa mara ya pili kwa mahakama kuu kufanya uamuzi kuhusu bondi ambayo hakimu amempa mshukiwa huyo.