Wadudu watumika kama kitoweo na wenyeji wa Congo
1st August, 2015
Taifa la Congo linatambulika kwa kula vyakula vya ajabu ajabu. Miongoni mwa vyakula hivyo ni pamoja na wanyama pori kama vile sokwe na hata tumbili. Si wanyama pekee, wenyeji wa Congo pia hula wadudu tofauti na bei ya kitoweo cha wadudu kuongezeka maradufu kuliko hata chakula cha kawaida.