Viongozi wa makanisa wampongeza Rais Uhuru kwa msimamo wake kuhusu swala la mashoga
27th July, 2015
Viongozi wa makanisa nchini wamepongeza msimamo wa Rais Uhuru Kenyatta kuhusiana na suala la haki za mashoga nchini. wakuu wa kanisa la Methodist kwenye hafla moja mjini siolo walisifia jawabu alilolotua rais kenyatta kwenye kikao mbele ya rais wa marekani Barack Obama wakisema kenya ni taifa lenye mila na desturi za kuheshimika zinazofaa kuhimizwa kote nchini