Gavana Cornel Rasanga atoa ombi kurai ziara ya Rais Obama kuelekea Siaya
20th July, 2015
Gavana wa Siaya Cornel Rasanga ametuma ombi maalum kwa ubalozi wa marekani nchini kenya akiurai kupanga ziara ya obama kuelekea kaunti hiyo….Rasanga ametangaza kuwa tayari wamefanya mazungumzo na kinara wa cord Raila Odinga kuhusu umuhimu wa Obama kuzuru kaunti za eneo la Nyanza ambalo ni chimbuko la Rais Obama….kauli hiyo pia imeungwa mkono na gavana wa Homabay Cyprian Awiti.