Muungano wa kitaifa wa vinywaji na pombe washtaki serikali kwa hasara waliopata
7th July, 2015
Zaidi ya shilingi billioni mbili zimepotea katika muda wa wiki iliyopita, haya ni kwa mujibu ya muungano wa kitaifa wa vinywaji na pombe - Nabak, ambao wamesema kuwa wafanyibiashara wengi wamepoteza mali ya mamilioni ya pesa katika shughuli ya juma zima ya kukabiliana na pombe haramu. Kauli hii inajiri huku maeneo tofauti yakiendeleza operesheni ya kumaliza pombe haramu, Hussein Mohammed anatupa taswira kamili ya swala hili huku mvutano huu ukionekana kufika mahakamani.