Hospitali ya Kapenguria inapokea watoto zaidi ya sabini walioathirika na utapia mlo
2nd July, 2015
Hospitali ya wilaya ya Kapenguria kaunti ya pokot magharibi inapokea watoto zaidi ya sabini walioathirika na utapia mlo kila mwezi. Ikiwa ndio kaunti inayoongoza humu nchini kwa asili mia 46 ya watu wanaoathirika na kufariki kufwatia athari za utapia mlo. Hata hivyo wanaume wamelaumiwa kwa kupuuza familia zao huku wakitumia wasaa wao kuchunga mifugo yao. Saida swaleh ameandaa makala yatakayoweka bayana changamoto za lishe kutoka kaunti ya pokot magharibi.