Idara husika za serikali zimetangaza kuwapokonya leseni kampuni za vileo
2nd July, 2015
Kufuatia agizo la jana la rais, idara husika za serikali zimetangaza kuwapokonya leseni wenye kampuni zote zinazotengeneza vileo ambavyo havitengenezwi katika viwanda maalumu hadi pale shirika la kuratibu ubora wa bidhaa nchini litakapo kakugua vileo hivyo na kuviidhinisha. Waziri wa usalama wa taifa joseph nkaiserry ametoa onyo kwa maafisa watakaoshindwa kudhibiti pombge haramu katika maeneo yao kwamba watafutwa kazi. Na kama anavyoarifu lofty matambo katika eneo la kati la nchi ulevi miongoni mwa wanaume unatishia kufelisha jamii.